Sunday 27 August 2017

NAIBU SPIKA WA BUNGE DKT. TULIA ACKSON KUKUTANA NA WASANII

Tanzania Music Foundation pamoja na NSSF wanakualika wewe msanii au mdau wa muziki katika mkutano mkubwa utakaoendeshwa na naibu spika wa bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson. Ni siku ya Jumamosi tarehe 02/09/2017 kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea. Kifungua kinywa pamoja na chakula cha mchana vitapatikana. Hii si ya kukosa kabisa kwani kutakuwa na fursa mbalimbali kwa ajili yako wewe msanii ama mdau wa muziki nchini. Mkutano utafanyika katika ukumbi wa NSSF Ilala jijini Dar es salaam. Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa nchi kukutana na wasanii kwani hivi majuzi waziri wa habari sanaa na michezo Dkt. Harison Mwakyembe pia alipata nafasi kama hii ya kukutana na wasanii.

No comments:

Post a Comment