Sunday 27 August 2017

MIONGONI MWA WASANII WATAKAOHUDHURIA MKUTANO WA NAIBU SPIKA WA BUNGE NI HAWA

Hawa ni kati ya wasanii ambao wamesema wanamuunga mkono naibu spika wa bunge Dkt. Tulia Ackson na watahudhuria katika mkutano mkubwa wa wasanii ambao utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 Agosti, 2017 katika ukumbi wa NSSF kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea.
Mh. Martha Mlata - Mbunge
Mzee Makasy
Rose Muhando
Dkt.Donald kisanga - Raisi TAMUFO
Stella Joel Msanii na Katibu wa TAMUFO
Masanja mkandamizaji
Emmanuel Mbasha
Edson Mwasabwite
Goodluck Gozbert
Christina Shusho
Upendo Nkone
Martha Mwaipaja
Madam Ruti
Jane Misso
Magreth Sembuche
Ani Annie
Tumaini Njole
Mess Chengula na wengine wengi

NAIBU SPIKA WA BUNGE DKT. TULIA ACKSON KUKUTANA NA WASANII

Tanzania Music Foundation pamoja na NSSF wanakualika wewe msanii au mdau wa muziki katika mkutano mkubwa utakaoendeshwa na naibu spika wa bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson. Ni siku ya Jumamosi tarehe 02/09/2017 kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea. Kifungua kinywa pamoja na chakula cha mchana vitapatikana. Hii si ya kukosa kabisa kwani kutakuwa na fursa mbalimbali kwa ajili yako wewe msanii ama mdau wa muziki nchini. Mkutano utafanyika katika ukumbi wa NSSF Ilala jijini Dar es salaam. Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa nchi kukutana na wasanii kwani hivi majuzi waziri wa habari sanaa na michezo Dkt. Harison Mwakyembe pia alipata nafasi kama hii ya kukutana na wasanii.

Monday 21 August 2017

BASATA WANAKUKARIBISHA KWENYE JUKWAA LA SANAA

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), leo tar 21/08/2017 linakukaribisha wewe mtanzania katika jukwa la sanaa litakalofanyika kuanzia saa 4 mpaka saa 7 mchana katika viwanja vya Basata. Mada kuu ya jukwa hilo ni Umuhimu wa wasanii kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, watoa mada ni PSPF, kwa maelezo zaidi waweza piga namba hii +255 715 973 952.  Wadau wote mnakaribishwa na Hakuna kiingilio

Friday 18 August 2017

VIONGOZI TAMUFO

Picha ya kumbukumbu ya viongozi wa Tamufo walipokutana katika Hoteli ya LANDMARK iliyopo
Mbezi beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Raisi Dkt. Donald Kisanga, katikati ni Katibu Bi. Stella Joel na kulia ni Dkt. Ezekiel Kyogo
Viongozi wa Tamufo

KATIBU WA TAMUFO BI. STELLA JOEL AKIWA NA BAHATI BUKUKU

Katibu wa Tanzania Music Foundation Bi. Stella Joel akiwa na mwanamziki nguli wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku, kwa pamoja walihudhuria katika mkutano mkubwa wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe hivi majuzi siku ya alhamisi tarehe kumi ya mwezi wa nane, Waziri alijadiliana kwa ukaribu na wadau wa muziki wa Injili jinsi ya kutatua kero zinazo wakabili na kuahidi kuzimaliza.
Bi. Stella Joel - Katibu wa TAMUFO ( Mwenye Nguo Nyekundu) akiwa na Bahati Bukuku ( Aliyevaa Miwani)

RAISI WA TAMUFO AKIHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE

Raisi wa Tanzania Music Foundation alipopata nafasi ya kuongea machache pamoja na wadau wenzake wa muziki wa Injili katika mkutano mkubwa wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe hapo majuzi siku ya alhamis tar 10/08/2017.
Dkt. Donald Kisanga (Raisi - Tamufo)

RAISI WA TAMUFO AFURAHIA UJIO WA WAZIRI DKT. HARRISON MWAKYEMBE

Raisi wa Tanzania Music Foundation Dkt. Donald Kisanga, amefurahia ujio wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe katika mkutano mkubwa wa wanamuzi, waandaaji na wadau wa muziki wa Injili nchini. Waziri huyo ametoa ahadi ya kuondoa kero mbalimbali zinazo wakabili wanamuzi wa Injili mpaka kukosa kunufaika na kazi zao, huku akipokea maoni na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau hao wa muziki wa Injili na kuahidi kushirikiana nao. Mkutano huo ulifanyika siku ya Alhamisi tarehe 10/08/2017 katika ukumbi wa NSSF ILALA JIJINI DSM

Raisi wa Tanzania Music Foundation (Mwenye tai nyekundu) katika picha ya pamoja akiwa na Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe.