Friday 18 August 2017

RAISI WA TAMUFO AFURAHIA UJIO WA WAZIRI DKT. HARRISON MWAKYEMBE

Raisi wa Tanzania Music Foundation Dkt. Donald Kisanga, amefurahia ujio wa Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe katika mkutano mkubwa wa wanamuzi, waandaaji na wadau wa muziki wa Injili nchini. Waziri huyo ametoa ahadi ya kuondoa kero mbalimbali zinazo wakabili wanamuzi wa Injili mpaka kukosa kunufaika na kazi zao, huku akipokea maoni na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau hao wa muziki wa Injili na kuahidi kushirikiana nao. Mkutano huo ulifanyika siku ya Alhamisi tarehe 10/08/2017 katika ukumbi wa NSSF ILALA JIJINI DSM

Raisi wa Tanzania Music Foundation (Mwenye tai nyekundu) katika picha ya pamoja akiwa na Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe.

No comments:

Post a Comment